Breaking




Thursday, 27 July 2017

HADITHI:UTAJIRI WA MZEE FISI






SEHEMU YA 1

Mzee fisi ni MTU maarufu nani tajiri sana katika kijiji cha mitini, lakini hakufurahia utajiri wake sikumoja akafunga safari kwenda kwa mganga wake wakienyeji kwenda kuongeza utajiri,alipofika kwa mganga akamkuta mganga wake lakini akampa mashariti ili aweze kuuongeza utajiri.

Mganga huyu alimpa shariti moja tu mzee fisi amtoe mtoto wake kafara ili awezekumpatia utajiri, Mzee fisi nae alikubali kumtoa mtoto wake kafara ili apate utajiri. Bahati mbaya mzee fisi alikuwa na mtoto mmoja tu katika familia yake alipomtoa mtoto wake no kweli utajiri uliongezeka na kuwa na Mali nyingi, mzee fisi alifurahi sana nakumshukuru mganga wake. Lakini Siku moja alikaa nakuanza kuwaza nakumkumbuka mtoto wake aliye mtoa kafara, ghafla akasikia sauti ikisema Mzee fisi umethamini Mali kuliko utu tena umemtoa mwanao kafara ili upate utajiri, Sasa nakwambia mzee fisi kuanzia Leo maisha yako yatakuwa magumu naya shida na hutakuwa tajiru tena.

Mzee fisi baada yakusikia sauti hii akajiuliza ni nani aliyeniambia maneno haya, Akafunga safari kwenda kumwambia mganga wake alipofika kwa mganga wake alikuta kaburi kwenye ule mji na mganga hakuwepo akaulizia kwa majirani wakamwambia Mganga alishafariki nakaburi lake ndo hilo hapo. Mzee fisi alilia sana nakuanza kusema mganga mganga umenidanganya kumbe nawewe huna uwezo wakunipa utajiri nasasa ushakufa nitafanya nini, baada yakuwaza haya yote akaamua kurudi nyumbani kwake akiwa anatembea kuelekea nyumbani kwake akaona moshi mkubwa unatokea kwajuu karibu na nyumbani kwake akasema moshi huu unatoka wapi. Akaendelea kutembea alipofika nyumbani kwake akaona nyumba yake yote imeungua kwa moto na Mali zake zote zimeteketea kwa moto, Mzee fisi akalia sana kwa uchungu akisema mtoto wangu nimemtoa kafara ili nipate utajiri lakini Mali zangu zote na nyumba yangu imeungua moto nitaishi kwa nani mimi na mtoto wangu nilimtoa kafara kwaajili yakupata utajiri na utajiri umeisha.................

Je Mzee fisi alipata pakuishi au hakupata na je alifanya nini baada ya hapo?

Usikose kusoma sehemu ya pili ya utajiri wa mzee fisi na Mwandishi wako. James Gerald.

Mawasiliano 0767472566.

No comments:

Post a Comment