![]() |
Oscar Bennedicto MD Wa Oscar Superlucky
Oscar Bennedictor Mpwelela alizaliwa Nachingwea Feb 2 akiwa ni mtoto wa kwanza kwenye famili ya watoto wanne ya Bennedictor Mpwelela ambae ni mmwera wa Nambalapala Nachingwea, ni Mkulima na mama ake Cellina Simon Manyanya ni mkulima pia.
Baada ya mama yake mzazi kuona uharaka wa uelewa wa Oscar, alimuanzisha shule akiwa mdogo sana na hatimae kumaliza elimu ya msingi akiwa na miaka 18 tu, akamaliza form four akiwa na miaka 24 mwaka 2009, sehemu zote hizo yeye ndio alikua mdogo kuliko wote darasani kuanzia Kawawa Primary School Liwale, Kawawa Secondary School.
![]()
Wakati akisubiri majibu, Oscar alijiunga na Babu Mzee Simon Manyanya Mzaa Mama Yake na kusomea ufundi wa kutengeneza tv, deck na radio masomo ambayo aliyamaliza na aliyasoma kwa sababu ilikua ni kazi ya pili aliyoipenda, baada ya hapo mama yake mzazi alishawishiwa na marafiki zake ili Oscar arudishwe shule kuendelea na masomo ya sekondari kitu ambacho alikikubali lakini hakikua na mapokezi mazuri kwa Oscar kwa sababu yeye alihitaji kufanya kitu kingine kwa wakati ule.
Mambo yalibadilika pale uncle wake aitwae Yusuph Manyanya aliekua Masasi aliporudi Liwale na kumshawishi mama Oscar amuache mtoto afanye kile anachotaka na anachokipenda, hapo ndipo Oscar akapata nafasi ya kwenda kujiunga na Southen Driving School Mtwara kusomea udereva.
Baada ya mwaka mmoja Oscar alijiunga na Sanaa kwa muda na akarejea Nachingwea April 2013 kutafuta kazi baada ya hali kuwa ngumu kwenye familia na kukosa pesa kwa ajili ya kujiendeleza na masomo.
Sanaa pamoja na website yake ya oscarsuperlucky.com ndio vilivyofanya ukubwa wa jina lake uongezeke Pia Oscar Kashashiriki Kucheza Baadhi ya Film Ikiwemo A HAVA 2015, JUU KWA JUU 2016, YATIMA 2016 nk. Chini Ya Production Ya Kaka Ake Fadhili Mandepe Iitwayo FAHARI MEDIA na Oscar Alikuwa Anafanyia Kazi Hapo Mwaka 2015
Shukrani za pekee kwa Mr Juma Mwitenda, Azimina Manyanya, Simon Manyanya, Cellina Manyanya, Edward Manyanya na Fadhili Mandepe ambao walikua kama wazazi/marafiki wakati Oscar akiwa Katika Hali Ngumu Ya Maisha Lakini Wao Walisimama Nae Imara.
Patrick Bennedictor, Bonnita Matias, Azah Juma Mwanja Hawa Ndio Ndugu Zake Oscar Na Mama Yao Anaitwa Cellina Simon Manyanya Kwa Sasa Wote Hawa Wana Kaa Liwale Lindi.. tunakutakia maisha marefu na maendele yako pia Mama Yetu Cellina Simon Manyanya Tunakupenda Sana..
|



Monday, 31 July 2017
OSCAR SUPERLUCKY HII HAPA JUU YA MAISHA YAKE.
Tags
# Kimataifa
# Udaku
About Unknown
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Udaku
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment