Breaking




Wednesday, 2 August 2017

AZAM YATOLEA UFAFANUZI SAKATA LA GADIEL MICHAEL KWENDA YANGA




 

Usiku August 1, 2017 kuna story imetrend sana kwenye mitandao ya kijamii ikimhusisha beki wa kushoto wa Azam na Taifa Stars kwamba, ameshasaini mkataba wa awali na mabingwa wa VPL Yanga lakini klabu yake ya sasa inamuwekea ‘kauzibe’.

Team Manager wa Azam FC Philip Alando amezungumza na kipindi cha Power Breakfast cha Clouds FM kutoa ufafanuzi juu ya suala la Gadiel Michael ambapo amesema, mchezaji huyo bado ni wa Azam na anamkataba na klabu hiyo.

“Gadiel Michael ni mchezaji wa Azam na kama mnavyojua alikuwa timu ya taifa na wachezaji wote waliokuwa timu ya taifa walipewa mapumziko maalum ya siku saba na walitakiwa kuungana wenzao Julai 30, 2017,” Philip Alando.

“Kama walivyofanya wenzake, Gadiel pia alikuja mazoezini Jula 30, nipende tu kuwajulisha kwamba Gadiel anamkataba na Azam kama kuna taratibu zozote za kumruhusu kwenda Yanga au timu yoyote anayotaka kwenda hizo zitafuatwa endapo wanaomuhitaji watafika ofisini na kuonana na uongozi.”

“Mimi kama team manager, watu wa Yanga walikuja jana walionana na Abdul Mohamed ambaye ndio General Manager wetu katika klabu ya Azam, walipewa maelekezo lakini kikubwa ni kwamba Gadiel Michael ni mchezaji wa Azam bado yupo Azam hadi pale maelezo mengine yatakapotolewa tofauti na hapo.”

”Toka awali siku zote na tutaendelea kuwa hivyo, Azam haijawahi kumzuia mchezaji wake kuondoka ikiwa taratibu zimefuatwa na nadhani Azam ndio klabu inayojitahidi kutokuwa na migongano baina ya mchezaji na klabu au klabu na klabu. Wameshaondoka wachezaji wengi kwa kufuata utaratibu, hata Yanga au klabu nyingine inayomuhitaji wakifuata utaratibu hatutakuwa na kinyongo Gadiel ataondoka kwenda kujiunga na hiyo klabu.”

No comments:

Post a Comment