Breaking




Saturday, 5 August 2017

SASA UNAWEZA KUOMBA HATI YA KISAFIRIA(PASSPORT) KUPITIA MTANDAO



UZINDUZI WA FOMU YA MAOMBI YA PASIPOTI MTANDAONI

(ONLINE PASSPORT APPLICATION FORM) 

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

                                                      IDARA YA UHAMIAJI      

TAARIFA KWA UMMA

KUZINDULIWA KWA HUDUMA YA FOMU YA MAOMBI YA PASIPOTI MTANDAONI (ONLINE PASSPORT APPLICATION FORM)

Idara ya Uhamiaji inapenda kuutangazia umma kuwa imezindua rasmi huduma ya fomu ya maombi ya pasipoti mtandaoni (Online Passport Application Form). Huduma hii inapatikana katika tovuti ya Idara kupitia link ifuatayo:https://www.immigration.go.tz/ppt_application/ na itaanza kutumika rasmi kuanzia siku ya Jumatatu tarehe 07 Agosti, 2017. 

Kufuatia kuzinduliwa kwa huduma hii, waombaji wote wa pasipoti wanashauriwa kuzijaza fomu hizo mtandaoni, Kisha kuzichapisha (Printing) na kuziwasilisha katika Ofisi za Uhamiaji.

Hata hivyo, matumizi ya huduma hii yataenda sambamba na huduma inayotumiwa sasa ya fomu za maombi ya pasipoti mpaka pale itakapotangazwa vinginevyo. 

Utaratibu wa namna ya kujaza fomu hizo umeelekezwa katika fomu husika mtandaoni, na pia wateja wanaweza kupata ufafanuzi au maelezo zaidi kuhusu huduma hiyo kupitia anuani ya Idara ambayo ni  info@immigration.go.tz au katika Ofisi yoyote ya Uhamiaji iliyo karibu nao. 

Taarifa zaidi kuhusu huduma hii zitaendelea kutolewa kupitia vyombo mbalimbali vya habari.

Imetolewa na:

KITENGO CHA UHUSIANO,

MAKAO MAKUU, IDARA YA UHAMIAJI,

04 AGOSTI, 2017.

VIDEO: JINSI RAIS MAGUFULI ALIVYOWAPATANISHA PAUL MAKONDA NA RUGE MUTAHABA WA CLOUDS MEDIA



No comments:

Post a Comment