Breaking




Friday, 4 August 2017

TFF YAKIRI KUIKOSEA YANGA,YAAHIDI KUIOMBA MSAMAHA




Klabu ya Yanga imesikitishwa na kitendo cha  Bodi ya Ligi ya TFF kutowaaliKa Yanga ktika hafla ya kugawa jezi za msimu ujao kwa klabu za ligi kuu  iliyofanyika jana.

Katika hafla hiyo ambayo Yanga hawakuhudhuria waliwakilishwa na Msemaji wa Simba Haji manara.

Klabu ya yanga imesikitishwa na kitendo hicho nakuitaka TFF iwaombe msamaha mara moja kwa sababu imewapotezea mapato pia imesababisha waonekane wazembe kwa kutohudhuria hafla hiyo hali ya kuwa hawakupewa taarifa. 

Kufuatia malalmiko hayo ya Yanga,Msemaji wa TFF Alfred Lucas amekiri ni kweli Yanga wana haki ya kulalamika kwasabbau hawakupewa taarifa kwa wakati.

"Ni kweli tuliokosea ni sisi TFF na hasa bodi ya ligi"

Allfred lucas amesema TFF wataiandikia barua Klabu ya Yanga kuiomba msamaha kwa kitendo hicho

No comments:

Post a Comment