Albert Msando
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe Dkt Harrison Mwakyembe ameunda kamati ya watu watano wakiongozwa na Mwanasheria Alberto Msando ya kujadili namna ya kutatua changamoto na matatizo yanayowakabiri Wasanii wa muziki wa kizazi kipya.
Majina hayo ya wanakamati yameteuliwa na wasanii wenyewe, Waandishi wa Habari pamoja na wadau mbalimbali walioalikwa kwenye kikao hicho cha kujadili changamoto za wasanii ili kero za wasanii na watayarishaji wa muziki ziweze kutatuliwa na Serikali.
Majina ya watu walioteuliwa kwenye kamati hiyo ni Rapa Azma Mponda, Nikki Wa Pili, Witness Kibonge na wengine ni Mtangazaji mkongwe Taji Liundi na Mwanasheria Alberto Msando aliyependekezwa moja kwa moja na Waziri Mwakyembe.
“Tumeunda Kamati hii ili iweze kuchanganua na kujadili changamoto zinazowakumba Wasanii na jinsi ya kuzitatua kisha tuzifanyie kazi sisi kama serikali kazi yetu ni kuhakikisha Wasanii wetu wanafanikiwa kwa kiwango kikubwa bila kuingiliwa na wanyonyaji wa kazi zenu”,amesema Mhe Dkt Mwakyembe
Hata hivyo waziri Mwakyembe ameomba Wasanii wa kizazi kipya kuwa wamoja katika mchakato huu na kuweka kando tofauti zao za zamani kama watataka kufanikisha hilo huku akiwataka BASATA wajirekebishe katika utendaji kazi wao.
No comments:
Post a Comment