Sungo blog
Frank De Boer amekuwa kocha wa kwanza kufukuzwa kazi msimu huu mpya katika ligi kuu ya England.
Imewachukua siku 77 pekee kwa Crystal Palace kumfukuza kazi kocha huyo baada ya kuifundisha Palace kwenye michezo minne ya ligi kuu ya England akiwa hajawahi kupata ushindi wowote huku mechi ya jana dhidi ya Burnley ikiwa ndiyo kichocheo cha moto wa kufukuzwa kuwaka na laiti kama angeshinda jana basi ingekua habari tofauti.
Frank alijiunga na Palace kabla ya kuanza msimu huu akichukua nafasi ya Sam Alladyce aliyeiokoa timu hiyo na janga la kushuka daraja.
Taarifa toka Vyombo vya habari nchini England hivi sasa vinaeleza kwamba kocha wa zamani wa England Roy Hodgson ndiye atayemrithi Frank De Boer na amesaini mkataba wa miaka miwili kuifundisha Crystal Palace.
No comments:
Post a Comment