Breaking




Saturday, 16 September 2017

DIWANI WA CHADEMA AFARIKI DUNIA

Sungo blog

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mbeya mjini kimepata pigo baada ya diwani wake wa Viti Maalumu, Ester Mpwiniza kufariki dunia.

Mwenyekiti wa Chadema Mbeya Mjini, Obadia Mwaipalu amesema Mpwiniza ambaye amewahi kuwa Mwenyekiti cha Baraza la Wanawake Mbeya mjiji (Bawacha)  amefariki muda mfupi baada ya kufikishwa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya kutokana na Shinikizo la damu.

"Kweli Kaka (mwandishi) Kamanda wetu wa nguvu ametutoka jana jioni nNi presha iliyoondoa uhai wake ghafla. Alidondoka nyumbani  na alipowahishwa Hospitali ya Rufaa hakuchukua muda akafariki," amesema Mwaipalu.

Amesema taratibu nyingine kuhusiana na msiba huo zinasubiri ndugu wa marehemu, ofisi ya Meya jiji la Mbeya pamoja na chama.

Ofisi ya Meya wa Jiji la Mbeya imewatangazia wananchi kwamba msiba shughuli zote za msiba zimehamia mtaa wa Ghana ambako itatoa taratibu nyingine baada ya viongozi kukutana.

Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Nyanda za Huu kusini, Mchungaji Peter Msigwa ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya marehemu, ofisi ya Meya jiji la Mbeya, Chadema Mbeya mjini na kwa wananchi wa Jiji la Mbeya.

"Aidha kwa niaba ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini (Nyasa) napenda kutoa pole kwa wana CHADEMA na wananchi wa Jiji la Mbeya ambapo marehemu licha ya kuwa alikuwa mwakilishi wa wananchi pia alijitoa sana katika shughuli za Chama’’amesema

Ameongeza kwamba Marehemu ni miongoni mwa waliongoza  operesheni mbalimbali zilizofanywa na Ofisi ya chama  Kanda ya Nyasa na pia enzi za uhai wake  aliweza alishika wadhifa  wa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Wilaya ya Mbeya Mjini.

‘’Niko Nairobi kwa ajili ya kumuuguza  Tundu Lissu lakini niko nanyi pamoja kwa maombi na nawasihi tuendelee na maombi mbalimbali kwa ajili ya kuliombea Taifa na majeruhi akiwemo Tundu Lissu" imesema sehemu ya taarifa ya Msigwa aliyoituma kupitia kwa mratibu wake, Emmanuel Masonga.

No comments:

Post a Comment