Sungo blog
Wikiendi imemalizika na watu wanarudi makazini, lakini mwishoni mwa wiki kulipigwa michezo mingi barani Ulaya na watu wakapiga na kupigwa, hivi ndio vipigo vikubwa vilivyotokea Ulaya wikiendi hii.
1.Watford 0 Man City 6. Hiki ndicho kipigo kikubwa zaidi mwishoni mwa wiki, ilikuwa ni Jumamosi katika Watford wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani wakakubali bao 6 kwa nunge toka City, wauaji walikuwa Kun Aguero aliyepiga 3, Gabriel Jesus, Benardo Silva na Raheem Sterling.
2.Napoli 6 Benevento 0.Driens Martens alifunga mara 3 wakati Napoli wakiichapa Benevinto, mabao mengine yaliwekwa kimiani na Lorenzl Insigne, Allan na Jose Callejon.
3.Borussia Dortmund 5 Koln 0. Walitoka kupigwa 3 na Arsenal katikati ya wiki lakini wanakubali tena kufa bao 5 mbele ya Dortmund huku Pierre Aubemayang na Maximilian Philip wakifunga mara mbili mbili huku Sorkatais akifunga lingine.
4.Manchester United 4 Everton 0. Timu za jiji la Manchester zinaongoza kutoa dozi kwani wakati City waliwaua Watford bao 6, majirani zao wa United waliipiga Everton bao 4 huku mabao yao yakiwekwa kimiani na Antonio Valencia, Henrikh Mkhitaryan, Romelu Lukaku na Anthony Martial.
5.Bayern Munchen 4 FSZ Mainz 0. Thomas Lewandoski alifunga mara mbili katika mchezo huu dhidi ya Mainz huku Thomas Muller na Arjen Robenn wakifunga mengine.
No comments:
Post a Comment