Sungo blog
Serikali ya Kinshasa yafahamisha kuanza uchunguzi baada ya kuuawa kwa wakimbizi 34 kutoka Burundi Kamanyola
Serikali ya Kinshasa yatangaza kuanza uchunguzi kufuatia vifo vya wakimbizi 34 kutoka nchini Burundi waliouawa kwa kupigwaa risasi Kamanyola Mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.
Kwa upande wake serikali ya Bujumbura iliitaka seriakali ya Kinshasa na Umoja wa Mataifa kutoa maelezo kuhusu tukio hilo.
Msemaji wa serikali ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo Lambert Mende amefahamisha kuwa serikali imeanzisha uchunguzi Jumamosi baada ya wakimbizi kufyatuliwa risasi Mashariki mwa DR Congo.
Taarifa zafahamishakuwa wanajeshi watano waliuawa na watu wanaodaiwa kuwa wakimbizi jambo ambalo linashangaza serikali ya DR Congo vipi wakimbizi wanaweza kuwa na silaha na kushambulia
No comments:
Post a Comment