Sungo blog
Tunakumbuka miaka kadhaa iliyopita,mwanasiasa machachari wa wakati ule chache wangwe,alipata ajali mbaya ya Gari wakati akitokea Dodoma kwenye vikao vyakibunge,njiani akiwa na dereva wake,inasemekana walipata ajali mbaya mno hali iliyopelekea ndugu wangwe kupoteza maisha,gari iliharibika vibaya sana ila upande wa dereva kutoka salama bila mkwaruzo wowotee mwilini,hali hii ilileta sintofahamu miongoni mwa watanzania,ukizingatia wakati ule ndugu wange hakuwa na maelewano mazuri na viongozi waandamizi wa chadema taifa,hasa katika kinyang'anyiro cha uongozi wa juu wa chama hicho.
Miaka kadhaa baadae mwanasiasa machachari wa upinzani Tundu lisu anapatwa na msukosuko wa shambulizi za risasi 32 zote zikiwa zimelenga kuupata mwili wake,bahati nzuri risasi chache ndizo ziliupata mwili wake na nyingi kupita mbali ya mwili, hali ambayo kila mmoja anaona ukuu wa Mungu katika jambo hili,chakushangaza katika tukio hili,ambalo lilimuhusu mheshimiwa lisu na dereva wake ambao wote walikuwa sehemu moja katika gari dereva hakudhurika hata kwakukwaruzwa na risasi hili linawezekanaje ingali lisu alikuwa mita chache kutoka alipokaa dereva?
Mazingaumbwe haya na ajali ya chacha mbona hayatofautiani?? Maswali yakujiuliza kwanini dereva asiumie kwa namna yeyote??
Muda utaongea hakuna jambo lisilo na mwisho ilitokea kwa wangwe dereva katoka mzima huku wangwe kapoteza maisha,ikatokea kwa lisu kwa bahati nzuri katoka majeruhi huku dereva katoka mzima wa afya bila mkwaruzo naamini siku moja ukweli utajualikana.
No comments:
Post a Comment