.
Sungo blog
Hospitali ya taifa Muhimbili imeongeza mashine za kusafishia damu kutoka 25 hadi 42 na kuongeza idadi ya watu wanaopata huduma hiyo kwa siku kutoka 68 hadi 136 huku ikitarajia kuanza huduma ya kupandikiza figo mwezi Octoba mwaka huu.
Daktari bingwa wa magonjwa ya figo wa hospitali hiyo Dkt. Onesmo Kisanga amesema tatizo la maradhi ya figo ni kubwa na kuongeza kuwa idadi kubwa ya wagonjwa wanafika hospitali wakiwa katika hali mbaya kutokana na watu kutokuwa na desturi ya kupima afya zao.
Kwa upande wake mkuu wa kitengo cha mawasiliano wa hospitali hiyo Bw. Aminiel Eligaeshi amesema uboreshaji huo umetokana na mahitaji makubwa yaliyopo ambayo yalikuwa hayalingani na vifaaa vilivyokuwepo awali na kwamba lengo la Muhimbili ni kutoa huduma zoteza kibingwa ili kuwapunguzia wagonjwa na serikali gharama za kwenda juzifuata nje ya nchi.
Katika tukio lingine mfuko wa pamoja wa maendeleo umetoa msaada wa shilingi bilioni 227.76 kwa wizara afya kwa ajili ya kuboresha huduma za afya ikiwemo ya mama na mtoto pamoja na chanjo ambapo katibu mkuu wa wizara hiyo Dkt. Mpoki Ulisubisya amesema kwa mara ya kwanza serikali itapeleka fedha hizo moja kwa moja kwenye vituo vya kutolea huduma.
No comments:
Post a Comment