Sungo blog
Geita. Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Musukuma, madiwani na baadhi ya wananchi wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Geita muda huu.
Kwa nyakati tofauti kuanzia Septemba 14 hadi 17 walikamatwa na polisi wakituhumiwa kuhusika kufunga barabara za kuingia kwenye mgodi wa dhahabu wa Geita (GGM).
Kwa sasa akina Musukuma wamehifadhiwa katika mahabusu ya mahakama wakisubiri kuingia kwenye chumba cha hakimu kusomewa shtaka linalowakabili.
Septemba 14 madiwani wa halmashauri mbili za Wilaya ya Geita walifunga barabara zinazoingia GGM wakishinikiza kulipwa Dola 12 milioni za Marekani zinazotokana na ushuru wa huduma.
No comments:
Post a Comment