Breaking




Saturday, 16 September 2017

MKAZI WA KIJIJI CHA NYAMBURI WILAYANI SERENGETI AMEGUNDUA ENEO LENYE AINA MBALIMBALI ZA MADINI

.

Sungo blog

Mkazi mmoja wa kijiji cha Nyamburi wilayani Serengeti mkoani Mara,amedai kugundua eneo lenye aina mbalimbali za madini huku akiomba serikali kulichukua eneo hilo kwa ajili ya kuchimbwa ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Rais Dk John Pombe Magufuli za kuhakikisha rasilimali za nchi zinatumika kwa maslahi ya taifa.

Akizungumza mbele ya uongozi wa kijiji hicho,mkazi huyo bw Petro Mwita,amesema kuwa baada ya kugundua madini hayo amekuwa akifanya juhudi za kukabidhi eneo hilo kwa serikali chini ya Rais  John Pombe Magufuli.

Hata hivyo Mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho cha Nyamburi wilayani Serengeti Bw Samson Matiko,amesema baada ya kushuhudia eneo hilo,tayari ametoa kibali kwa mwananchi huyo ili aweze kufikisha suala hilo kwa uongozi wa wilaya kwa hatua zaidi.

Mkuu wa wilaya ya Serengeti Bw Nurdin Babu,akizungumza na ITV kwa njia ya simu, amekiri kupata taarifa hizo,lakini amesema suala hilo limekuwa likishughulikiwa na katibu tawala wa wilaya hiyo na kuomba kupewa nafasi ili aweze kulizungumzia.

No comments:

Post a Comment