Breaking




Friday, 8 September 2017

TUNDU LISSU AMEPELEKWA KENYA KUPATA MATIBABU ZAIDI

Sungo blog



Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu aliondoka katika uwanja wa ndege wa Dodoma usiku wakuamkia leo kwenda Nairobi kwa ajili ya matibabu.

Lissu ambaye alijeruhiwa akiwa kwenye gari nyumbani kwake Area D, mjini Dodoma baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulika.

Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini amesema, katika safari hiyo Lissu ameambatana na mkewe, madaktari wawili wasio na mipaka, Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe na Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa.

Selasini amesema kuwa Lissu anapelekwa katika Hospitali ya Aga Khan mjini Nairobi.

Ndege hiyo iliyombeba ya 5H-ETG imeondoka katika Uwanja wa Dodoma saa sita na robo usiku.

No comments:

Post a Comment