
Na. Oscar Bennedictor, Lindi.
Serikali wilayani Kilwa mkoa wa Lindi imehaidi kufanyia marekebisho tuta linalozuia maji kutoka bahari ya Hindi yasiingie kwenye eneo linalotumika kwa shuguli za kilimo katika kijiji cha Songomnara.
Ahadi hiyo ya serikali imetolewa leo na mkuu wa wilaya hiyo, Christopher Ngubiagai, kijijini Songomnara alipozungumza na wananchi wanaoishi katika kijiji hicho. Ngubiagai ambae kabla ya kuzungumza na wananchi hao alilazimika kutembea kilometa 16 kwa miguu katika pwani ya bahari ya Hindi akiwa na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya na viongozi wa serikali ya kijij hicho ilikujionea hali halisi ya pwani hiyo, alisema serikali italifanyia marekebisho tuta hilo lililojengwa na baadhi ya asikari waliopigana vita kuu ya pili ya dunia kwa kushirikiana na wananchi 117, mwaka 1962.
Alisema wananchi wametimiza wajibu wao, kwahiyo niwajibu wa serikali kuunga mkono juhudi hizo. “Ukiondoa mbali kuzuia maji ya bahari kuingia kwenye eneo linalotumika kwa shuguli za kilimo, lakini pia hili ni eneo la kihistoria. Sisi kama serikali niwajibu wetu kutunza maeneo aya kwa kushirikiana nanyi ili baadae yawe miongoni mwa vivutio vitakavyotuingizia mapato,” alisema Ngubiagai.
Mkuu huyo wa wilaya mbali nakuhaidi kuliboresha tuta hilo alitumia hadhara hiyo kuwaasa wananchi wakijiji hicho takribani 480 kutunza, kulinda na kuhifadhi Mali kale zilizopo katika maeneo yao. Huku akiwakumbusha viongozi wa serikali za vijiji kuwashirikisha wananchi katika kupanga shuguli za maendeleo zinazowahusu.
“Washirikisheni wananchi kuwapa taarifa za miradi inayotekelezwa katika vijiji vyenu. Wasomewe taarifa za mapato na matumizi. Miongoni mwa kero ni wananchi kutoshirikishwa, wanaona tu miradi inatekelezwa katika vijiji vyao”, alisisitiza Mkuu huyo wa wilaya ya Kilwa.
Kuhusu changamoto za umeme, maji na huduma za afya, Ngubiagai aliwaondoa hofu wananchi hao kwa kuwahaidi serikali itashugulikia changamoto hizo. Kwamadai kwamba serikali iliyopo niyao na ipo kwa ajili ya kuwatumikia. Bali moyo wakujitolea walioonesha waendelee nao katika kuibua na kanzisha miradi ya maendeleo na huduma za jamii ili serikali iwaunge mkono.
Wilaya ya Kilwa ni miongoni mwa wilaya chache zilizona vivutio vya utalii nchini. Ikiwamo magofu ya kale yaliyopo Kilwa Kisiwani na Songomnara. Magofu ambayo shirika la Sayansi, Elimu na Utamaduni la umoja wa mataifa limeyatangaza kuwa ni miongoni mwa urithi wa dunia.
No comments:
Post a Comment