Breaking




Wednesday, 20 September 2017

UPDATE: IDADI YA WALIOFARIKI YAPINDUKIA 150 MEXICO.


Sungo blog

Tetemeko la ardhi lenye nguvu ya 7.1 kwenye kipimo cha Richter lilmekumba Jumanne hii Septemba 19 nchi ya Mexico na kusababisha vifo vya watu 224, kulingana na idadi ya mwanzo iliyotolewa na maafisa wa serikali

Tetemeko hilo limezua hali ya sintofahamu na watu kuwa na wasiwasi mkubwa katika nchi hiyo yenye wakazi milioni 20. Ni miaka 32 sasa tangu tetemeko jingine lenye nguvu lililoua zaidi ya watu 10,000 mwaka 1985.

Idadi ya watu waliopoteza maisha ni 224. Kwa mujibu wa kituo cha Marekani cha utabiri wa mambo ya tetemeko (US Geological Center USGS), kitovu cha tetemeko hiulo kilikua kimepatikana katika jimbo la Puebla, katika katikati mwa nchi, karibu na mji mkuu, kilomita 51 za kina.

Tetemeko hilo limedondosha karibu majengo 30 katika mji mkuu wa Mexico city.

Watu wanaotoa huduma za dharura wakisaidiwa na mamia ya watu wanaojitolea bado wanaendelea kutafuta manusura ambao wamefukiwa na kifusi.

Tetemeko lauwa 140 mexico...

No comments:

Post a Comment