SUNGO BLOG
KESI ya Naibu Waziri wa Fedha wa zamani, Adam Malima na dereva wake, RamadhanMohammed, ya kuzuia Polisi kutekelezamajukumu yao na kushambulia, imeahirishwahadi Novemba Mosi mwaka huu.
Kesi hiyo iliyopo katika Mahakama ya HakimuMkazi Kisutu, imeahirishwa baada ya upandewa mashtaka kuieleza mahakama hiyo kuwashahidi aliyetakiwa kutoa ushahidi hakupatamwaliko kwa wakati licha ya kuwepo kwashahidi mwingine mahakamani hapo.
Wakili wa Serikali, Patrick Mwita, akisaidianana Glory Mwenda, alidai Mahakamani hapombele ya Hakimu Mkazi Mkuu, RespiciusMwijage, kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili yakuendelea na ushahidi na tayari walikuwa nashahidi Mwita Joseph, lakini kutokana na asiliya kesi hilo, aliyepaswa kutoa ushahidialitakiwa kuwa Daktari Mchwempaka kabla ya Joseph.
Kutokana na maelezo hayo, Hakimu MkaziMkuu, Mwijage aliahirisha kesi hiyo hadiNovemba Mosi mwaka huu itakapoendelea naushahidi.
Katika hati ya mashtaka, Malima anadaiwakuwa Mei 15, mwaka huu katika eneo la Masaki kwa makusudi alimzuia ofisa wa polisi mwenye namba H.7818 PC Abdul kufanya kazi yake halali wakati alipokuwa akimkamata kwa kupaki vibaya gari lake alimshambulia na kumsababishia maumivu
No comments:
Post a Comment