RAIS WA TFF ATINGA
Sungo blog
Rais Wa Shirikisho La Soka Nchini Tanzania Wallace Karia Pamoja Na Kaimu Katibu MkuuKidao Wilfred Wametembelea Makao MakuuYa Shirikisho La Soka Barani Afrika Caf NaKukutana Na Rais Bw. Ahmad Ahmad.
Ziara Hiyo Ya Rais Karia Imefanyika JanaAmbapo Walitua Kwenye Ofisi Za Caf ZilizopoCairo Nchini Misri Na Kupokelewa Na RaisAhmad Ahmad Kisha Kufanya Kikao Kilichojadili Maendeleo Ya Soka Nchini.
Aidha Kikao Hicho Kilihudhuriwa Pia Na Rais Wa Heshima Wa Tff Ambaye Ni Mjumbe Wa Kamati Ya Utendaji Ya Caf, Bw. Leodegar Tenga.
Rais Wa Caf Ameahidi Kuisaidia Tff Katika Mipango Ya Maendeleo Ya Soka Nchini Ili Kuongeza Umoja Kwasababu Soka Siku Zote Hujenga Umoja Na Mshikamano.
Rais Karia Na Wenzake Waliingia Madarakani August 12 Mwaka Huu Ambapo Tangu Waanze Majukumu Yao Wamekuwa Wakijitahidi Kuhakikisha Soka Linapiga Hatua Kwa Kutafuta Wadhamini Ambao Watawezesha Maendeleo Hayo Ya Soka.
No comments:
Post a Comment