Breaking




Wednesday, 20 December 2017

BARCELONA KUSHITAKIWA NA ATLETICO MADRID

Sungo blog


Klabu ya Atletico Madrid ya Hispania inapanga kuishtaki Barcelona kwa shirikisho la soka ulimwenguni (Fifa) kujaribu kutaka kumsajili Antoine Griezmann katika njia ambayo siyo sahihi.

Inadaiwa kuwa wiki iliyopita Rais wa Barca, Josep Maria Bartomeu aikutana na baadhi ya watu wa familia ya Griezmann kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya kumnasa mchezaji huyo.

Griezmann alisaini mkataba mpya na Atletico Madrid msimu uliopita ambao utafika kikomo mwaka 2021.

Kwa mujibu wa sheria za Fifa zinasema endapo timu ikiwa inataka kumsajili mchezaji lazima iwasiliane na klabu yake anayoichezea kabla ya kuruhusiwa kufanya mazungumzo. Endapo FIFA itabaini kuwa Barca wamefanya kosa hilo wanaweza kufungiwa kufanya usajili katika kipindi cha msimu mmoja mpaka miwili.

No comments:

Post a Comment