Breaking




Monday, 18 December 2017

RAIS MAGUFULI AMUONGEZEAMUDA KINANA

Sungo blog

Katibu mkuu wa Chama  Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana leo ameteuliwa na Mwenyekiti wa Chama hicho, Rais John Pombe Magufuli  kuendelea kuwa katika nafasi yake kwa kipindi kingine.

Akiongea katika mkutano wa 9 wa Chama hicho unaoendelea mkoani Dodoma amemshukuru kwa kazi yake nzuri  kwa muda wote ambao amekuwa  katika nafasi hiyo huku akiweka wazi kuwa ni lazima aendelee kufanya nay kazi kwasababu ameridhishwa na utendaji wake wa kazi.

''Namshukuru ndugu Kinana kwa msaada wake mkubwa alionipa kwa kipindi chote hicho nafikiri  anafaa kuendelea kuwa katika nafasi hiyo kwa kipindi kingine,'' amesema Magufuli. Kauli ya Rais Magufuli inaondoa tetesi zote zilizokuwa zinadai kuwa Kinana ameandika barua ya kuomba kujiudhuru katika nafasi yake kwa kilichodaiwa kuwa haridhishwi na utendaji wa Mwenyekiti wake Rais Magufuli.

No comments:

Post a Comment