Breaking




Wednesday, 27 December 2017

RAIS WA TFF,WALLACE KARIA APIGA MARUFUKU MASHINDANO YA NDONDO,LIGI ZA WABUNGE


Sungo blog



Sungo blog.Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia amefuta mashindano yoyote ya soka yaliyo nje ya mfumo wa shirikisho hilo isipokuwa tu kwa kibali maalum.

Karia amesema kwamba mashindano ya soka yasiyo rasmi kama ambayo huandaliwa na wanasiasa majimboni na hata na baadhi ya taasisi na wadau, yamekuwa yakipewa umuhimu mkubwa kuliko mashindano rasmi ya TFF zikiwemo ligi.

Karia amesema wakati umefika sasa Wabunge, wanasiasa na wadau kwa ujumla watoe fedha kuzidhamini timu za majimboni mwao badala ya kuanzisha mashindano ya ng’ombe na mbuzi.


No comments:

Post a Comment