Breaking




Monday, 25 December 2017

Tetesi za usajili Ulaya: Pesa za wachina za mvuta Marouane Fellaini.


Sungo blog

December 26, 2017

0 COMMENTS

Dirisha la usajili katika nchi za ulaya linafunguliwa wiki moja kutoka sasa, na hizi hapa ni tetesi za usajili zilizojiri na  kutokea mwezi Januari.

Marouane Fellaini,30, anajiandaa kuondoka katika klabu ya Manchester United wakati huu ambapo vilabu vya nchini Uchina vimeonyesha nia ya kutaka huduma ya kiungo huyu wa Kiberigiji. Katika klabu ya Manchester United hapati nafasi ya kutosha pamoja na kuwa majeruikwa sasa.

Mkurugenzi wa klabu ya Borrusia DotmundJoachim Hans- Watzke amekanusha taarifa zilikuwa zinamuhusu kiungo mshambuliaji wa klabu ya Manchester United, Henrikh Mkhitaryan kuwa yupo katika rada za timu hiyo kutokana na kutotengamaa kwa uchumi wa timu ya Dotmund.

Delli Alli atakuwa tayari kujiunga na klabu ya Real Madrid ama Barcelona kama timu moja wapo itamhakikishia nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza. Klabu ya Real Madrid inahusishwa na kumsajili mshambuliaji huyo raia wa Uingereza.

Kocha wa klabu ya Crystal palace, Roy Hodgson ameanza kuhofia klabu hiyo itamuuza staa wake Wilfred Zaha kutokana na ukata wa pesa katika klabu hiyo.

No comments:

Post a Comment