Breaking




Saturday, 6 January 2018

BOCCO NAHODHA MPYA SIMBA SC

Sungo blog


Faridi Miraji.                                                             

Klabu ya Simba kupitia kwa Kocha anayekaimu ukocha mkuu Masoud Djuma imemthibitisha rasmi kuwa John Bocco sasa ndio Nahodha wa Simba Sc  na atasaidiwa na Hussein Mohamed 'Zimbwe Jr' na Mwinyi Kazimoto.

Simba wamefanya hivyo Baada ya Kuachana na Beki wa kimataifa wa Zimbambwe, Method Mwanjale ambaye ndio alikuwa nahodha wa kikosi hicho akisaidiwa na Hussein Mohamed na John Bocco. 

Kwenye mechi dhidi ya Mwenge kitambaa ya unahodha alivaa Hussein Mohamed huku John Bocco alianzia Bechi na aliingia kipindi cha pili ila Hussein Mohamed aliendelea kuvaa kitambaa cha unahodha yakaibuka maneno kuwa Hussein hajamheshimu Bocco kama nahodha mkuu kuendelea kukivaa kitambaa cha unahodha na Bocco akiwa uwanjani. 

Klabu ya Simba kupitia kwa meneja wa timu hiyo wametoa ufafanuzi kuwa John Bocco na Hussein Mohamed wote walikuwa manahodha wasaidizi tangu aondoke Mwanjale walikuwa bado hawajateua nahodha mkuu wa klabu hiyo ndipo jukumu hili walimpa kocha Masoud Djuma kiteua.

Pia Klabu ya Simba imemrejeshea unahodha wake Mkongwe Mwinyi Kazimoto baada ya kumvua msimu uliopita. Msimu uliopita nahodha wa Simba alikuwa Jonas Mkude akisaidiwa na Mwinyi Kazimoto. Ila kwenye maandalizi ya msimu huu Simba waliteua manahodha wapya Mwanjale, Bocco, na Hussein Mohamed leo tena wamemrejeshea unahodha wake Mwinyi Kazimoto

No comments:

Post a Comment