Breaking




Sunday, 14 January 2018

RAIS MAGUFULI AVUNJA UKIMYA KUHUSU KUONGEZA MIAKA 7 MADARAKANI

Sungo blog



Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzaania na mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM),Mh. Dkt.John Pombe Magufuli jana tarehe 13-01-2018 amekutana na kufanya mazungumzo na katibu waHalmashauri kuu ya CCM ,Itikadi na na uenezi Ndg;Humphrey Polepole,Ikulu jijini Dar es salaam.

  
Baada ya mazungumzo na Ndg Polepole amesema Mhe.Dkt.Magufuli amemuelekeza kuwajulisha wanachama wa CCM na umma wa Watanzania kuwa anasikitishwa na hafurahishwi na mjadala naoendelea juu kuongezwa kwa kipindi cha urais kutoka miaka 5 iliyonwekwa kwa mujibu wa katibu,hadi miaka 7. 


Ndg.Polepole amesema Mhe.Dkt,Magufuli amewataka wanachama wa CCM na umma  wa Watanzania kwa ujumla kuupuuza mjadalahuo  kwa kuwa haujawahi kujadiliwa katika kikao chochote cha chama,nani kinyume na katiba ya CCM na katiba ya nchi.

No comments:

Post a Comment