Breaking




Monday 26 June 2017

Kassim Mganga Anyoosha Maelezo juu ya kufanya Kazi na WCB

Unapomzungumzia tajiri wa mahaba kwa hapa bongo basi unakila sababu za kumtajaKassimu Mganga aliyeachia ngoma yake siku ya jana aliyomshirikisha Baby J kutoka pande za Zanzibar.Hivi si unaikumbuka ile taarifa ya Kassimu Mganga kujitoa Tip top Connectioninayosimamiwa na Babu Tale ambae pia ni meneja wa WCB. Sasa taarifa hii inakuhusu.
Oscarsuperlucky.co.tz inakuthibitishia kuwa, licha ya Kasimu na Tale kutokuwa kwenye kazi ya Lebo wawili hao wamekuwa na ukaribu zaidi tofauti na mwanzo jambo ambalo tumeweza kuliona kwenye ngoma ya Kassimu Mganga kusimamiwa na WCB kwenye soko la mauzo.
Oscarsuperlucky.co.tz imeinyaka nukuu kamili ya tajiri huyo kutoka mandhabei akinyoosha maelezo jinsi Babu Tale anavyo mhendo kwa sasa.
“Japo niliondoka Tiptop Connection lakini mimi na Babu Tale bado tulikiwa tunashirikishana kwa mambo mengi sana na nimepata nafasi ya kuwa katika app yao ya Wasafi.com hivyo amezidi kuniweka karibu zaidi na yeye japo kuwa mimi nina management yangu” alisema Kassim Mganga.

No comments:

Post a Comment