Breaking




Monday 26 June 2017

KAYA 90 ZAPEWA ZAWADI YA SIKUKUU LIWALE.

Mkuu wa wilaya ya Liwale,mhe. Sarah Chiwamba (kushoto) akimkabidhi bibi Zawadi wa chakula kwa ajili ya sikukuu ya idd el fitri. 
Na: Oscar Bennedictor | Liwale-Lindi. Tz.
Mkuu wa wilaya ya Liwale akiwa na baadhi ya akina mama waliweza kupata msaada siku ya jumamosi 24 mwaka 2017.
Mkuu wa wilaya ya Liwale akiwa na baadhi ya akina mama waliweza kupata msaada siku ya jumamosi 24 mwaka 2017. 
     Kaya zilizofika kupokea msaada wa chakula kwa ajili ya sikukuu ya idd el fitri 
Mkuu wa wilaya ya Liwale mkoani Lindi,mhe. Sarah Chiwamba ametoa msaada wa chakula kwa kaya 90 zinazoishi katika mazingira magumu wilayani Liwale kwa ajili ya sikukuu ya idd el fitri.
Akikabidhi msaada huo jumamosi juni 24, 2017 alisema kuwa msaada alioutoa ni  mchele kilo 270,maharage kilo 90 pamoja na mafuta lita 90 kwa kaya 90.
Mkuu huyo wa wilaya alisema ametoa msaada huo baada ya kuguswa na kaya hizo zinazoishi katika mazingira magumu na kuziunga mkono ili kuweza kusherekea sikukuu ya iddi kama familia zingine zinazojiweza.Chanzo. 

No comments:

Post a Comment