Breaking




Friday 7 July 2017

NDEMLA AWAITA MEZANI YANGA, ADAI YUPO TAYARI KUJIUNGA NAO




KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Said Ndemla, amesema ataondoka Msimbazi baada ya kumaliza mkataba wake Machi mwakani.

Ndemla ameweka wazi kuhusiana na maisha katika klabu ya Simba ambaye hivi karibuni alihusishwa kujiunga na watani wao wa jadi Yanga.

Akizungumza  jana, Ndemla alisema amezikaribisha klabu zitakazomhitaji ikiwamo Yanga kuanzia kipindi cha dirisha ndogo la usajili,  kwani atakuwa amebakisha miezi minne mkataba wake kumalizika.

Ndemla alisema safari yake ya kuondoka Simba itaanza kipindi hicho cha usajili kutokana na sasa hawezi kuondoka Msimbazi kwa kuwa bado ana mkataba mpaka Machi mwakani.

Alisema pamoja na kuwepo kwa taarifa za kutakiwa katika timu nyingine lakini kwa sasa hawezi kufanya mazungumzo na klabu nyingine hadi pale kandarasi yake itakapobakia miezi sita.

“Nipo Simba na msimu unaokuja wa Ligi Kuu Tanzania Bara nitaendelea kuwapo,  lakini nitaweka wazi kama nitaondoka au la baada ya kumalizika mkataba wangu, timu yoyote inayonihitaji isubiri kwanza,” alisema Ndemla

No comments:

Post a Comment