Breaking




Tuesday 4 July 2017

"Nilishamtosa na kumpotezea Q chief" - Chid Benz

Rapa Chid Benz leo ametoa siri kuwa wimbo wake mpya 'muda' ambao ameshirikiana na Q Chief haukuwa katika mipango yake na kudai Q Chief alikuwa akimlazimisha kufanya ila yeye alikuwa hataki na alishamtosa Q Chief.
Rapa Chid Benz

Chid Benz amesema hayo alipokuwa kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio na kusema hakutaka kurekodi wimbo huo kwa sababu mpaka wanakutana na Q Chief tayari alikuwa na ngoma nyingi ndani.
"Kiukweli kabisa mimi nilikuwa sitaki kufanya kazi na Q Chief sababu muda ambao tumekutana tayari nilikuwa na ngoma kama mia tatu ndani hivyo sikuwa na haja ya kurekodi kazi nyingine, kwa hiyo nilimuacha studio na kumwambia afanye kazi nitarudi lakini wakati huo mimi nilikuwa nishampotezea nikijua hiyo kazi sitafanya ", alisimulia Chid Benz.
Rapa huyo anadai bila ya ushawishi mkubwa wa Q Chief wimbo huo wa 'muda' huenda usingetoka maana yeye hakuwa na lengo la kufanya kazi na Q Chief na wala hakuwa na mpango wa kuachia wimbo kama huo.
"Chillah alinishikilia sana, nilipomkimbia akanipigia simu tena na kuniita niende studio, nilipofika nilisikia ile kazi ndiyo nikasema ngoja niandike sasa mistari hivyo niliandika tu dakika kadhaa nikamaliza nikaingia studio nikarekodi, baada ya hapo mimi niliiacha hiyo kazi wao ndiyo wakafanya kila kitu nyuma, kwa hiyo haukuwa kwenye mpango wangu kabisa",alisisitiza Chid Benz. 

No comments:

Post a Comment