Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amezungumza mambo mbalimbali akiwa katika ziara mkoani Singida na leo amezindua barabara ya Manyoni – Itigi – Chaya yenye urefu wa KM 89.3.
Tazama nukuu zake hapa:
-Kabla sijaongea chochote naomba tuwaombee Mashujaa wetu walioitetea nchi yetu. Naomba tuiname tuwaombee.
-Watanzania naomba tuwe tunakumbuka mahali tulipo toka, mahali tulipo na mahali tunapoelekea.
-Tanzania ninayoipenda ni Tanzania yenye umoja, Tanzania yenye upendo, Tanzania inayomtanguliza mbele Mungu.
-Tunataka tuwe na umeme wa uhakika ili tuweza kuwa na Tanzania ya viwanda tunayoitaka.
-Wakati wa kukaa kwenye magenge na kushinda kwenye pool kukaa kupiga stori kwamba tutaletewa chakula cha bure, hakuna.
-Utajiri hautakuja kwa wavivu, lazima niwaeleze ukweli. Niwaombe wana Itigi wakati wa kukaa kwenye magenge umepita.
-Mimi ndiye Rais, hakuna anaejua siri za Serikali kama Rais. Leo mmepata Rais anaewaambia ukweli.
-Kosea hata kuoa, utatoa hata talaka ila usije ukakosea kuchagua.
-Ukiona mtu anapiga kelele wananchi wake waendelee kuwa masikini ujue amemeza kitu ndani.
-Kazi ya kutumbua ni ngumu unaweza ukajikata, unaweza ukarukiwa na usaa . Inadepend hilo jibu limekaa sehemu gani.
-Na leo watoto wote wanakalia madawati awe wa Chadema awe wa Tundu Lissu anakaa.
-Ni mataifa machache duniani yanayosomesha watu wake bure, hata Ulaya hawafanyi hivyo ndugu zangu.
-Ndege ya abiria 262 yenye uwezo wa kusafiri moja kwa moja kutoka Marekani inakuja mwakani.
-Waliojenga kwenye hifadhi ya reli waanze kujiandaa kisaikolojia, wanaweza kuanza kubomoa taratibu nyumba zao.
-Ma-DC na Ma-RC, sitoi chakula kama kwako kuna njaa, wilaya ikiwa na njaa wewe DC hufai kuwa DC, na wewe RC hufai.
-Nataka Tanzania iwe kama Ulaya. Tutafika tu lakini tutabanana.
– TanRoadS ni ya 3 kwa uchapaji kazi Afrika.
-Suala la ubinafsishaji mimi silipendi kabisa, siwezi nikawalaumu waliofanya hivyo, lakini kuacha kusema siwezi.
-Nikiondoka mimi hakuna atakayekuwa kama mimi, nasafisha njia ya Rais atakayekuja






No comments:
Post a Comment