Breaking




Thursday 6 July 2017

SIKU MBILI ZA HALIMA MDEE RUMANDE OYSTERBAY


 

Usiku wa kuamkia leo tarehe 6 Julai, 2017 ni usiku wa pili wa kulala korokoroni Mwenyekiti wa BAWACHA taifa, Mjumbe wa Kamati Kuu na Mbunge wa Kawe CHADEMA Halima James Mdee.

Katika rumande ya Polisi Oysterbay wilayani Kinondoni, Mdee ameendelea kutumikia masaa 48 aliyopewa na Mkuu wa Awilaya ya Kinondoni Ally Hapi kwa kosa la kumdhihaki Mh. Rais Dr. John Magufuli na kutoa maneno machafu yanayoweza kuvunja amani.

MATAMSHI YA MDEE
Akizungumza na waandishi wa habari Makao makuu ya CHADEMA Mdee ananukuliwa kudai kuwa Mh. Rais Magufuli amekua na "tabia ya hovyo...", "...ipo siku ataagiza watanzania (wake kwa waume) watembee vifua wazi...". Maneno mengine ni "...Rais lazima afungwe breki...",apewe semina elekezi n.k.

UCHOCHEZI
Halima Mdee anatajwa kutoa kauli za uchochezi kama vile "...woga wetu wananchi ndio unaotugharimu nchi hii..." "...watakaomfunga breki ni nyinyi wananchi...", maneno yanayotajwa kupandikiza na kuhamasisha chuki na vurugu kwa wananchi.

KUKAMATWA KWAKE
Baada ya amri ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mdee alianza harakati za kutoroka na kuruka mtego wa Polisi. Hata hivyo Jeshi la Polisi Kinondoni lilimkamata akiwa amejificha nyumbani kwa mama yake Kibamba wilayani Ubungo tayari kwa kutoroka.

RUMANDE
Halima Mdee anatajwa kuhifadhiwa katika rumande ya watuhumiwa wa uhalifu wa jinsia ya kike katika kituo cha Oysterbay Kinondoni.

BUNGE KUMUWAJIBISHA TENA
Akiwa bado anatumikia kifungo cha kutohudhuria Bunge hadi mwaka 2018, Halima Mdee ameingia tena matatani.

Kufuatia matamshi ya Mdee na waandishi wa habari Makao Makuu ya Chadema, Spika wa Bunge Job Ndugai ameagiza kamati ya Kinga na Madaraka ya Bunge kukutana haraka kujadili kitendo cha Mbunge huyo kutoa matashi ya kulifedhehesha Bunge. Akikutwa na hatia huenda akaongezewa adhabu nyingine

No comments:

Post a Comment