Nimeona niandike hili baada ya kuona wengi mkihangaikia kozi za kusoma vyuoni. Iwe diploma au digrii, kuna kozi binafsi sishauri kusomwa na wenye mkondo kama wangu (low and middle family class).
Utajiuliza, mie ni nani hata nishauri? Mimi ni Jumong wa Jf. Nilisoma mchepuo wa sayansi pale Tosamaganga. Nilipomaliza nilifaulu vizuri kwa division ya juu. Issue ikaja nikasomee nini chuo? Nikapata mshauri ambaye naye alisoma kozi asiyokusudia chuo. Aisee, nilitoka kwenye mabaioloji nikasoma uchumi chuo, niliteseka japo nilifaulu kwa mbinde. Kuja mtaani nilipata ajira ila I was not compitent and happy at all. Baada ya miaka kadhaa niliacha kazi nikarudi chuoni kada ya afya. Yaani ile shule nilikuwa so happy na nilifaulu vzr.
So, nashauri fanya uchaguzi mzuri aisee. Kozi kama;
Cultural helitage
Tourism
Hotel management
Statistics
Political science
Commuty development
Rural development
Kozi za mafuta na gas
Wildlife management
....
Na nyinginezo (TUONGEZEE) nashauri unapoenda kusoma, pima mbele zitakusaidiaje hasa kwenye ajira au kujiajiri. Wengi tunahitaji kuajiriwa, so chagua kozi itakayokupa mawanda mapana. Kozi nyingine mtaani wako kibao na wengi huishia kufanya kazi zisizo zao. Wengi huishia uanaharakati thanks God wengine wanakuwa WAJASILIAMALI. Kama unahitaji mkopo wa bodi pia kuwa makini. Kozi nyingine loan ni 0%. Kama unatoka familia kama yangu, fikiri kabla ya kutenda. Chuoni sio sekondari, na sio sifa kuwa chuoni tu, that is the determinant ya maisha. So ni bora usiende kupoteza muda.
Usiangalie sijui mzee fulani kasomea Marine leo anaendesha VX na ana ghorofa na mazagazaga kibao ukafikiri na wewe utatusua kwa kozi ya Marine...kila mtu ana mkondo wake!!
NB: HAKUNA RAHA KAMA KUSOMEA KILE UKIPENDACHO. HATA KAZI UTAIPENDA PIA.
Wasalaam
REPOST FROM JF







No comments:
Post a Comment