Breaking




Sunday, 13 August 2017

ALICHOSEMA RAIS WA FIFA BAADA YA WALLACE KARIA KUCHAGULIWA KUWA RAIS WA TFF




Muda mfupi baada ya Kamati ya Uchauzi Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania kumtangaza, Wallace Karia kuwa ndiye rais mpya wa TFF,  rais Shirikisho la soka duniani( FIFA),  Gianni Infantino ametuma salamu zake za pongezi.

Hayo yameelezwa na rais wa TFF, Wallace Karia wakati alipopewa nafasi ya kuzungumza kwa mara ya kwanza mara baada ya kukalia kiti hicho kilikuwa kimeachwa wazi na Jamal Malinzi.

“Kwanza nipende kumshukuru Mwenyezi mungu kwa kufanikisha yote na washukuru wajumbe wa Mkutano Mkuu kwa imani mliyo hionyesha kwangu nideni kubwa sana nawaahidi sitawaangusha”, amesema Karia rais wa TFF.

Wallace Karia ameongeza kuwa “Muheshimiwa Waziri na wasaidizi wako nawashukuru kwa kutusaidia katika kipindi hiki kigumu tulichopitia, kutoka FIFA na Caf tunawashukuru kwa uwakilishi wenu na mmesimama na kuangalia zoezi letu hadi kufikia hapa nadhani mtakuwa ni mabalozi wazuri kwa utaratibu ambao tumeufanya na demokrasia ambayo imefanyika hapa kuwa na kupeleka salamu hizi”.

“Lakini pia nipende kuwaambia wajumbe wa Mkutano Mkuu muda mfupi nimeongea na rais wa FIFA,  Infantino na ametupongeza kwa maamuzi haya amesema yupo tayari na atashirikiana na sisi kwa maswala yote ya maendeleo katika kuhakikisha tunaendeleza soka letu”.

“Wakati huo huo rais wa Caf, Ahmad Ahmad amepiga simu naye yeye ameeleza hayo hayo na amefurahi sana anamategemeo makubwa katika kuendeleza soka letu sina mengi ya kuongea zaidi ya kuwashukuru lakini nipende kuwaambia tu hii furaha iyende kuwa furaha ya kazi”.

No comments:

Post a Comment