Basi la Kampuni ya AM lililokuwa linatoka Mugumu Serengeti kwenda Mwanza limepata ajali katika Kijiji cha Bokore wilayani hapa na kujeruhi watu watatu.
Basi hilo lilikuwa na abiria zaidi ya kumi.
Polisi wilayani hapa wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo jana Alhamisi alfajiri ya saa 12.35 na kwamba wanamshikilia dereva kwa mahojiano.
Mganga mkuu wa Hospitali teule ya wilaya, Emiliana Donald amethibitisha kumpokea majeruhi mmoja aliyemtaja kwa jina la Sosoni Philipo mkazi wa wilayani Serengeti.
Amesema majeruhi huyo alikuwa analalamika kupata maumivu sehemu ya mgongo na kuwa wanaendelea na tiba.
Hata hivyo, majeruhi wengine wametibiwa katika zahanati za watu binafsi na kuendelea na safari zao.
No comments:
Post a Comment