Sungo blog
Godbless Lema,Mbunge wa Arusha Mjini
Jeshi la polisi wilaya ya Arusha mjini limezuia mikutano ya mbunge wa Arusha Mjini,Godbless Lema iliyopangwa kufanyika kuanzia kesho Jumpili Agosti 27 hadi 01 Septemba 2017.
Kupitia barua iliyoandikwa na Jeshi la Polisi kwenda kwa mbunge huyo wa Arusha,Polisi imesema wamezuia kufanyika kwa mikutano hiyo kwa sababu ya maandalizi ya mitihani ya darasa la saba na ujuio wa mwenge wa uhuru.
"Ofisi ya mkuu wa polisi wilaya ya Arusha inakutaarifu kuwa imezuia mikutano yako yenye ratiba ya kuanzai Tarehe 27.08.2017 hadi 01.09.2017 kwa sababu zifuatazo"
"1.Maandalizi ya kuhitimisha mitihani ya darasa la saba na mwenge wa uhuru ambayo ni matukio makuu ya kitaifa kwa tarehe hizo.Kwani baadhi ya viwanja vilivyopo kwenye ratiba yako ya mikutano navyo viko kwenye maandalizi kwa ajili ya mojawapo ya matukiohayo" . Ilieleza barua hiyo.
Aidha jeshi la polisi limemshauri mbunge huyo kufanya mikutano hiyo kuanzia tarehe 08.09.2017 baada ya matukio hayo muhimu kumalizika.
"Kwa sababu hizo unashauriwa kupanga mikutano muda wowote baada ya mitihani ya darasa la saba yaani kuanzia tarehe 08.09.2017". Ilieleza barua hiyo
Hii hapa chini barua iliyoandikwa na jeshi la polisi kwenda kwa mbunge huyo






No comments:
Post a Comment