Michuano ya Ndondo Cup msimu wa nne imehitimishwa leo Jumapili August 13, 2017 kwa mchezo wa fainali kati ya Goms United dhidi ya Misosi FC mechi iliyochezwa kwenye uwanja wa Kinesi.
Misosi FC wameibuka mabingwa wapya wa Ndondo baada kuifunga Goms kwa mikwaju ya penati baada ya sare ya kufungana 1-1 katika dakika 90 za kawaida.
Misosi walianda kupata goli la kuongoza ambalo lilidumu kwa dakika zaidi ya 70 za mchezo lakini Misosi wakasawazisha kwa kutumia makosa ya golikipa wa Goms.
Katika hatua ya changamoto ya penati Misosi wakaichapa Goms kwa jula ya penati 5-4 na kubeba ndoo ya Ndondo ikiwa ni mara yao ya kwanza.
Mechi ya fainali imeshuhudiwa na Naibu spika wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Tulia Ackson, Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Ally Hapi, Mbunge wa Mtama Nape Nnauye na wadau mbalimbali wa soka.
Misosi wamevuna kitita cha shilingi milioni 10 kwa kuwa mabingwa wa Ndondo Cup huku Goms wakijichukulia shilingi milioni tano baada ya kuwa washindi wa pili wa mashindano.
No comments:
Post a Comment