Saturday, 5 August 2017

KAPOMBE APELEKWA NDANDA KWA MKOPO




Beki wa kati wa Azam, Abbas Kapombe.

 

BEKI wa kati wa Azam, Abbas Kapombe amepelekwa kwa mkopo Ndanda FC ya Mtwara kwa ajili ya kukuza kiwango chake licha ya kupandishwa katika timu ya wakubwa hivi karibuni.

Kapombe ambaye alikuwa ni nahodha wa timu ya vijana ni miongoni mwa wachezaji sita waliopandishwa msimu huu kutoka katika timu ya vijana akiwemo, Abdul Haji, Godfrey Elias, Ramadhan Mohamed, Stanslaus Ladislaus na Yahaya Zaid.

Beki huyo mwenye uwezo wa kucheza nafasi ya kiungo mkabaji ameliambiaChampioni Jumamosi kuwa: “Ni kweli nakwenda kucheza kwa mkopo kwenye timu ya Ndanda, uongozi na mwalimu wameona nifanye hivyo ili niweze kukuza kiwango kabla ya kuanza kuitumikia timu ya wakubwa.”


No comments:

Post a Comment