AFP
Mtu moja ameuawa baada ya gari kugonga kibanda cha kituo cha mabasi kwenye mji ulio kusini mwa Ufaransa wa Marseille.
Dereva wa gari hilo amekatwa. Polisi wanasema kuwa haijulikani ikiwa gari hilo liliendeshwa makusudi kwenda kwa kibanda hicho au ni ajali ya kawadia.
- Dereva aliyewagonga na kuwaua watu 13 Barcelona asakwa na polisi
- Watu 13 wauawa na mamia kujeruhiwa, Barcelona
Lakini kuna ripoti kuwa kibanda kingine cha kituo cha mabasi kwenye wiliya tofaua kiligongwa mapema.
Polisi wamewashauri watu kuchukua tahadhari.
REUTERS
Vyombo vya habari nchini Ufaransa vinasema kuwa mwanamke ambaye aliuawa alikuwa wa umri wa miaka 40 hivi na dereva alikuwa mwanamume wa miaka 35 na alikuwa akifahamika kwa polisi.
Hakuna taarifa kamili kuhusu lengo ya kisa hicho.
Mwaka uliopita mjini Nice, zaidi ya watu 80 waliuawa wakati lori liliendeshwa kwenda kwa umati uliokuwa ukisherehekea, shambulizi ambalo Islamic State ilidai kutekeleza.






No comments:
Post a Comment