Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, ametoa wito kwa wakala wa usajili wa uzazi na vifo (RITA) kuhakikisha inawapatia vyeti vya kuzaliwa wakazi wote wa mkoa wake ambao hivi sasa ni asilimia 40 tu miongoni mwao ndiyo wenye vyeti hivyo.
Makonda aliyasema hayo leo wakati anazindua mfumo wa teknolojia, habari na mawasiliano (Tehama) wa usajili ambao utatumiwa na Rita. Akihimiza kutekelezwa kwa haraka kwa usajili hasa wa uzazi, aliwaomba wananchi kuwa wepesi wa kuwapa majina watoto wao wanaozaliwa ili waweze kurahisisha zoezi la watoto hao kupewa vyeti vya kuzali.
Alisema hilo wakati akielezea kwamba utamaduni wa wazazi kuchelewa kuwapa majina watoto, husababisha kuchelewa kwa mtoto kupewa cheti cha kuzaliwa mapema. Mkuu huyo alisisitiza kwamba kutekelezwa vyema kwa usajili huo kutatoa fursa zaidi kwa wazawa kufaidi fursa ambazo hapo awali zilikuwa zinatumiwa na watu ambao si raia wanaoishi kinyemela nchini.
No comments:
Post a Comment