Rais wa Misri, Abdel Fattah Al Sisi atua katika ardhi ya Tanzania kwaajili ya ziara ya kikazi ambapo amepokelewa na Mwenyeji wake ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli.
Rais Magufuli amempokea Rais huyo katika uwanja wa ndege wa Mwl Julius Nyerere ambapo ameongozana viongozi mbalimbali wa Kiserikali akiwemo Makamu wa Rais, Bi Samia Hassan Suluhu na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Rais wa Zanzibar.
Rais huyo yupo nchini Tanzania kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.
No comments:
Post a Comment