Baada ya Shirikisho la soka barani UlayaUEFA leo Alhamisi ya August 24 2017 mjini Monaco Ufaransa kuchezesha droo ya hatua ya makundi ya UEFA Champions League msimu wa 2017/2018, walitangazwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa Ulaya 2016/2017.
Nahodha wa timu ya taifa ya Urenoanayeichezea Real Madrid Cristiano Ronaldo ametangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa Ulaya 2016/2017 kwa kumshinda mpinzani wake mkubwa Lionel Messi wa FC Barcelona na golikipa wa JuventusBuffon.
Kutoka kushoto ni Messi, Buffon na Ronaldo
Ronaldo kwa msimu wa 2016/2017 ambapo ameshinda pia tuzo ya mshambuliaji bora 2016/2017, alikuwa na msaada mkubwa kwa club yake yaReal Madrid msimu uliyomalizika lakini ameifungia magoli 12 na kutoa assist 6 katika michuano ya UEFA Champions League.






No comments:
Post a Comment