Naona Sasa tumevuka mipaka kama tumeanza kuligusa na kutoa maneno ya dhihaka dhidi ya wapiganaji wetu yaani majeshi yetu ktk mitandao.
Najua ktk utendaji wa kazi yoyote ile mapungufu hayakosekani lakini si mpaka ifike hatua ya kutoa maneno ya dhihaka dhidi majeshi yetu na hata maneno Makali zaidi.
Tukumbuke Majeshi yetu ndiyo yanatufanya tuishi Salama kama nchi kwa kufanya kazi usiku na mchana.
Nadhani Kuna u muhimu wa kuangalia jinsi ya kutoa maoni namna ya kuboresha Majeshi yetu lakini si kwa dhihaka kama ninavyoona.
Majeshi yakigawanyika hakuna atakayebaki Salama.Tuwatie moyo na kuwapenda kwa kazi ngumu wanayoifanya ktk ulinzi wa Taifa Majeshi yetu yote.







No comments:
Post a Comment