Breaking




Friday, 25 August 2017

Simba Sc yamtega OMOG , yampa mechi za nne


                  


 Baada ya mashabiki wa timu ya Simba kumlalamikia Kocha wao kuwa timu inacheza kiwango cha chini na kupata ushindi mwembamba , Uongozi wa simba umeibuka na kumtetea Kocha huyo mcameron na kusema wacha wamtazame kwenye michezo kadhaa ya ligi kuu ili kusibitisha uwezo wake wa kufundisha club hiyo inayohitaji mafanikio makubwa msimu huu baada ya kukosa vikombe kwa misimu kadhaa.

Licha ya kuwa na wachezaji wengi wazuri na wenye uwezo, lakini timu hiyo bado imekuwa ikipata ushindi mwembamba kwenye mechi zake mbalimbali za kirafiki na Ngao ya Jamii, uliochezwa juzi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na Simba kuibuka washindi kwa mikwaju ya penalti 5-4 baada ya sare ya 0-0 kwenye muda wa dakika 90.

Moja wa kiongozi wa juu wa klabu hiyo, alisema kuwa kocha huyo si mbaya ila anaponzwa na mfumo anaotumia pamoja na majeruhi waliopo kwenye timu ambao kwa asilimia kubwa anawategemea.

“Omog kwa sasa ana kikosi kipana, ila ameshindwa kupata mabao mengi kutokana na mfumo anaotumia, mfumo wake ni wakuzuia zaidi, alafu kutokuwepo kwa John Bocco, Shomary Kapombe na Nilocas Gyan, kumekuwa ni tatizo kwake.

“Watu wanatakiwa kumpa muda, wasubiri wachezaji wote warejee kwenye timu hapo ndipo wataanza kupata mabao, tumpe hata mechi tatu au nne za ligi tutaanza kuona matunda yake,” alisema kiongozi huyo.

Simba wanafungua ligi kesho na Ruvu Shooting, watafuata kucheza na Azam FC, Mwadui FC na Mbao FC.

Alisema hata hivyo, walikuwa wanafikiria kumtafutia wataalamu wa soka, ili waweze kumshauri Omog juu ya mfumo anaotumia, kwa kuwa kocha huyo ni msikivu atawaelewa.

“Viongozi tumekubali kutomwingilia kocha katika kazi yake, ila tutamtafutia wataalamu kwa ajili ya kuongea naye zaidi juu ya kikosi hicho,” alisema kiongozi huyo.

Hata hivyo, Tuliamua kumtafuta Mkurugenzi wa Ufundi wa Timu hiyo, Mohamed Hussein (Muddy Kigoma), alisema kuwa kocha wao ni mzuri watu wamuache afanye kazi yake.

“Mmeanza maneno yenu, kocha wetu ni mzuri mwacheni afanye kazi yake, msianze kumchanganya,” alisema Hussein.

Simba msimu huu imesajili wachezaji wapya 12 kwa ajili ya kuboresha kikosi chao, nia ni kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu walioukosa kwa misimu minne mfululizo.

No comments:

Post a Comment