HALI YA MAJERUHI KATIKA KLABU
Klabu ya Simba Kupitia kwa Afisa Habari wake Haji Sunday Manara akiongea na msindiforums.com amesema Simba Wachezaji wake wako fiti kasoro mchezaji Shomari Kapombe ambaye Niye Majeruhi.
Lakini Kapombe anaendelea Vizuri na ameanza mazoezi Mepesi, " Kikosi chetu kipo vizuri Kasoro Shomari Kapombe ambaye bado anauguza Majeruhi ila naye anaendelea Vizuri " Alisema Manara.
ERASTO NYONI HAYUPO KAMBINI ILA LEO NDANI YA NYUMBA
Mchezaji Kiraka Erasto Nyoni kwasasa hayupo Kambini lakini Siku ya leo atajiunga na Wenzake, Nyoni ameenda Burundi kwenye Msiba wa baba mkwe wake Lakini ndugu msomaji wa Kwataunit.com leo atarudi kambini na Kuendelea na majukumu yake.
JUUKO MURSHID
Yule Beki wa Kati wa Uganda Cranes (Timu ya taifa ya Uganda) na Beki wa Simba Juuko MURSHID Ndugu msomaji wa Msindiforums ameonekana akifanya Mazungumzo na Mohammed Dewji kuna Taarifa zilisema Beki huyo huenda Akatimkia Orlando Pirates lakini Kiuhalisia Bado anamkataba Simba.
Taarifa za Ndani zinadai ndugu msomaji wa msindiforums.com wameshamalizana na Simba na Huenda akaendelea Kuitumikia Simba.






No comments:
Post a Comment