Baada ya Klabu ya Yanga jana kukubali kipigo cha penati 5-4 dhidi ya watani zao Simba SC klabu hiyo imekubali matokeo na kuwashukuru mashabiki zao ambao wamekuwa wakiwasapoti mara kwa mara na kudai mchezo ulikuwa mzuri japo hawakuwa na bahati.
Taarifa iliyowekwa katika ukurasa wa Yanga SC imewapongeza wachezaji wake kwa kiwango kizuri walichokionyesha ndani ya dakika 90.
"Ulikuwa mchezo mzuri, kiwango kizuri baada ya dakika 90, penati hazikuwa upande wetu. Asanteni 'fans' kwa sapoti pamoja na umoja wenu na upendo "
Pamoja na ujumbe uliotolewa na klabu ya Yanga , Naye Nahodha wa timu hiyo Haroub Cannavaro Jana alinukuliwa akisema kuwa wanachoangalia ni jinsi ya kuweza kuongoza ligi kuu inayoanza siku za karibuni."Vijana wangu wamejitahidi sana japokuwa bahati haikuwa ya kwetu. Nawapongeza kwa kazi kubwa waliyofanya lakini matuta ni mchezo wa kubahatisha na bahati wamepata Simba na ninawapongeza. Tunachotazama sasa mbele ni ligi kuu.
Kwa upande mwingine, msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mwaka 2017/2018 unatarajiwa kuanza Agosti 26 mwaka huu siku ya Jumamosi kwa kucheza vilabu mbalimbali vinavyoshiriki Ligi kuu kwa mwaka huu.
Ujumbe wa Yanga kupitia mtandao








No comments:
Post a Comment