Mwalimu wa fani ya elektroniki kutoka Mamlaka ya elimu na mafunzi ya ufundi (Veta) kituo cha Kipawa jijini dar es Salaam, Aneth Mganga, amegundua teknolojia mpya ambayo itakuwa mwarobaini kwamadereba pikipiki ambao hawapendi kuvaa kofia ngumu.
Kwa kutumia teknolojia hiyo, mwendesha poikipiki asipovaa kofia ngumu, basi pikipiki anayotaka kuiendesha haitawaka.
Kwa mujibu wa mwalimu huyo, teknolojia hiyo mpya haipatikani mahali pengine popote duniani.
Akizungumza katika banda la veta katika maonesho ya Nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Ngongo, mkoani Lindi, mwalimu Aneth amesema mfumo huo ukianza kutumika utapunguza madhara yanayotokana na ajali za pikipiki.
“uzuri wa teknolojia hii ni kuwa hata anapokuwa katika mwendo, dereva akivua tu kofia ngumu, pikipiki inazima,” anafafanua mwalimu Aneth.
Amesema kwa upande mwingine teknolojia hiyo inazuia wizi wa pikipiki kwa sababu mwizi hatoweza kuiwasha pikipiki hiyo mpaka awe na kofua ngumu ambayo imeunganishwa kielektroniki na pikipiki husika.
Mwalimu Aneth ameiomba serikali na wadau mbalimbali kuunga mkono ili kueneza teknolojia hiyo na kusaidia kampeni zirtakazoifanya ikubalike katika miongoni mwa waendesha pikipiki katika maeneo mbalimbali nchini.
Akielezea juu ya gharama ya vifaa vinavyotumika kutengezeaa kifaa hicho, mwalimu Aneth alisema kuwa kwa sasa vifaa hivyo vinapatikana nje ya nchi na anatumia fedha nyingi kuviagiza kwa sababu huagiza vichache.
“Naamini kama utawekwa utaratibu utakaowezesha kuviagiza kwa wingi, bei yake itapungua sana,” amesema.
No comments:
Post a Comment