Ikiwa zimepita siku mbili tangu jukwa la wahariri kumfungulia kifungo mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda cha kutoripotiwa na chombo chochotecha habari cha hapa nchini,lakini imeonekana kama vyombo vya habari vinaendeleza mgomo baridi wa kumsusia Rc Makonda.
Tangu jana nimejaribu kupitia magazeti mbalimbali na Kutazama/Kusikiliza TV/Radio bado nimeona suala hilo halijapewa uzito kwenye vyombo hivyo.
Lakini pia leo Agosti 11 nilitegemea magazeti kuandika habari kubwa ya jana ambayo Paul Makonda alitangaza kugawa miguu bandia kwa walemavu wa miguu,Gazeti moja tu la habari leo ambalo ni la Serikali ndiyo limeandka habari hiyo.
Hii inatokana na sintofahamu iliyotokea juzi ambapo baadhi ya waandishi wa habari hawakuridhishwa na kauli ya Rc Makonda ya kusema hatokaa kuwaomba msamaha kwa kutukio la Kuvamia CLoud Media.
Jukwaa la wahariri limeitisha kikao kingine siku ya Jumapili Agosti 11 kwa ajili ya kuliangalia upya suala hilo.
No comments:
Post a Comment