Tuesday, 19 September 2017

USIYOYAFAHAMU KUHUSU OSCAR SUPERLUCKY HAYA HAPA.

Related image

         Oscar Superlucky



Oscar Superlucky [ Bennedictor ] ni Mtangazaji na Mwandishi wa habari kutoka Tanzania na huripoti matukio yote ya ndani na nje ya Tanzania kila siku kupitia TWITTER, FACEBOOK, INSTAGRAM YOUTUBE (@oscarsuperlucky) na kwenye oscarsuperlucky.blogspot.com

Oscar Bennedictor Mpwelela alizaliwa Nachingwea Feb 2 akiwa ni mtoto wa kwanza kwenye famili ya watoto wanne ya Bennedictor Mpwelela ambae ni mmwera wa Nambalapala Nachingwea, ni Mkulima na mama ake Cellina Simon Manyanya ni mkulima pia. Baada ya mama yake mzazi kuona uharaka wa uelewa wa Oscar, alimuanzisha shule akiwa mdogo sana na hatimae kumaliza elimu ya msingi akiwa na miaka 18 tu, akamaliza form four akiwa na miaka 24 mwaka 2009, sehemu zote hizo yeye ndio alikua mdogo kuliko wote darasani kuanzia Kawawa Primary School Liwale, Kawawa Secondary School.

Image result for oscar superlucky

 Wakati akisubiri majibu, Oscar alijiunga na Babu Mzee Simon Manyanya Mzaa Mama Yake na kusomea ufundi wa kutengeneza tv, deck na radio masomo ambayo aliyamaliza na aliyasoma kwa sababu ilikua ni kazi ya pili aliyoipenda, baada ya hapo mama yake mzazi alishawishiwa na marafiki zake ili Oscar arudishwe shule kuendelea na masomo ya sekondari kitu ambacho alikikubali lakini hakikua na mapokezi mazuri kwa Oscar kwa sababu yeye alihitaji kufanya kitu kingine kwa wakati ule. Mambo yalibadilika pale uncle wake aitwae Yusuph Manyanya aliekua Masasi aliporudi Liwale na kumshawishi mama Oscar amuache mtoto afanye kile anachotaka na anachokipenda, hapo ndipo Oscar akapata nafasi ya kwenda kujiunga na Southen Driving School Mtwara kusomea udereva. 

Image result for oscar superlucky

Baada ya mwaka mmoja Oscar alijiunga na Sanaa kwa muda na akarejea Nachingwea April 2013 kutafuta kazi baada ya hali kuwa ngumu kwenye familia na kukosa pesa kwa ajili ya kujiendeleza na masomo. Sanaa pamoja na website yake ya oscarsuperlucky.com ndio vilivyofanya ukubwa wa jina lake uongezeke Pia Oscar Kashashiriki Kucheza Baadhi ya Film Ikiwemo A HAVA 2015, JUU KWA JUU 2016, YATIMA 2016 nk. 


Chini Ya Production Ya Kaka Ake Fadhili Mandepe Iitwayo FAHARI MEDIA na Oscar Alikuwa Anafanyia Kazi Hapo Mwaka 2015 Shukrani za pekee kwa Mr Juma Mwitenda, Azimina Manyanya, Simon Manyanya, Cellina Manyanya, Edward Manyanya na Fadhili Mandepe ambao walikua kama wazazi/marafiki wakati Oscar akiwa Katika Hali Ngumu Ya Maisha Lakini Wao Walisimama Nae Imara. Patrick Bennedictor, Bonnita Matias, Azah Juma Mwanja Hawa Ndio Ndugu Zake Oscar Na Mama Yao Anaitwa Cellina Simon Manyanya Kwa Sasa Wote Hawa Wana Kaa Liwale Lindi.. tunakutakia maisha marefu na maendele yako pia Mama Yetu Cellina Simon Manyanya Tunakupenda Sana..

Image result for oscar superlucky

Camera man / Location Manager and Actor / at Fahari Media & Oscar Superlucky Blog
Lives in Dar es salaam
Birthday: February 2

1 comment: