Breaking




Monday 9 October 2017

ALLY HAPI APIGANIA VIKOBA ENDELEVU

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapiameuomba uongozi wa Vicoba endelevunchini kutanua mtandao ili uweze kuwafikiawananchi wengi zaidi wakiwamo walimupamoja na wafanyabiashara ndogondogo.

Alisema ikiwa hayo yatafanyika itasaidiakuhakikisha Serikali inafikisha lengo lake lakuyakomboa makundi hayo kiuchumi.

Hapi alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaammwishoni mwa wiki wakati akizindua taasisiya Buta-Vicoba Endelevu iliyopo Bunju.

“Niwaombe sana viongozi wa Vicoba mtanuezaidi mtandao wenu ili muwafikie maelfuzaidi ya wafanyabiashara ndogondogo,wafanyakazi mbalimbali wa Serikaliwakiwamo walimu na mshirikiane nao katikakuangalia namna bora zaidi ya wao kupatahuduma za kifedha ikiwamo mikopo iliwaongeze thamani ya mitaji yao,’’ alisisitiza.

Akitoa taarifa ya hali ya vicoba nchinirais waVicoba EndelevuDevotha Likokola alisemamtandao huo unahusisha vikundi zaidi ya 100,000 vikiwa na wanachama zaidi ya 2,200,000 huku wakiwa na akiba ya zaidi ya Sh1 trilioni.

“Nitoe wito kwa wanajamii wazidi kushirikikatika Vicoba Endelevu kwa kuwa ni mfumoambao tayari umeonyesha kuwa unawezakuwaondoa katika umaskini,” alisema.

Akizungumza katika uzinduzi huo,mkurugenzi wa Buta-Vicoba Endelevu,Semeni Gama alisema taasisi hiyo inahusishavikundi 128 kutoka mikoa mbalimbaliikiwamo MbeyaKigoma, Lindi, Tanga naNjombe ikiwa na wanachama 2,186.

No comments:

Post a Comment