Breaking




Thursday 5 October 2017

CARVAJAL KUTANGAZA KUSTAAFU SOKA

Sungo blog


                         

Beki wa timu ya Real Madrid Dani Carvajal,25  kesho jioni  atatangaza kusitafu soka kutokana na matatizo ya moyo aliyoyapata hivi karibuni. Kutokana na hilo klabu ya Real Madrid itamtangaza Kuwa mjumbe wa heshima wa klabu hiyo na ataendelea kulipwa kila wiki. 

Dani Carvjal Baada ya kufanyiwa vipimo aligundulika na maambukizi ya virusi vinavyoshambulia ukuta uliozunguka moyo  ( viral pericardium infection). Taarifa kutoka Real Madrid inasomeka hivi

," Baada ya kufanyiwa vipimo  Dani Carvajal, aligundulika na maambukizi ya virusi vinavyoshambulia ukuta uliozunguka moyo " 

Lakini Real Madrid waligoma kubonyeza kitufe cha hofu (Panic Button) ambacho ni hatari zaidi kwa maisha ya Dani.  na wamesema  hawatosajili beki mwingine majira ya baridi . Madrid wanataka Nacho awe mbadala wa Carvajal pindi  Marcelo na Theo Hernandez watakapopona, lakini kwa muda huu beki chipukizi wa Morocco Achraf Hakimi hatokuwa na presha yoyote ya kuziba pengo la Carvajal.


No comments:

Post a Comment